Kitulo FM

Dc makete awatahadharisha wananchi uwepo wa mvua za El Nino

19 September 2026, 4:51 pm

pichani ni mkuu wa wilaya pamoja na mwenyekiti wa halmashauri kwenye zoezi la usafi hii leo

katika kuahakikisha mazingira yanakuwa safi katika mazingira yanayotuzunguka hii leo wananchi wameungana na mkuu wa wilaya ya makete katika kuhadhimisha siku ya usafi duniani kwa kusafisha mitaro ya maji jambo ambalo ni muhimu ili kuweza kuepukana na magonjwa na hata madhara ambayo yanweza kujitokeza wakati wa mvua ambazo zinatarajiwa kunyesha mwezi ujao

na mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Makete,  Mhe. kissa Gwakissa Kasongwa, amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuhakikisha kwa wanachukua tahadhari juu ya uwepo wa Mvua kubwa ya El Nino, kutokana na kuwepo kwa viashiria vya kuwepo kwa mvua hiyo kubwa kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA ambazo zinatarajiwa kuanza mwezi oktoba 2026.

Mhe. Kissa Kasongwa, amesema hayo leo  Septemba 19,2026, wakati akiongea na wakazi Makete eneo la Soko kuu, mara baada ya Kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani, ambayo yamefanywa kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Iwawa.

cue….. sauti ya kissa kasongwa

ni zoezi la usafi likiendelea kata ya iwawa

Katika kuhakikisha zoezi la usafi linazingatiwa kwa kiasi kikubwa mkuu wa wilaya mhe Kissa ameanzisha shindano ambalo litahusisha mitaa ndani ya kata ya iwawa ambayo itaweka mazingira safi pamoja na vyoo bora lakini pia soko lenye  choo safi watapewa zawadi  lengo ni kuendelea kuhamasisha usafi wa mazingira unazingatiwa kwa kiasi kikubwa katika makazi ya watu na hata kwenye maeneo ya biashara

Cue………saiti ya mhe kissa

Diwani wa kata ya iwawa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya makete mhe Rabson Mahenge amemshukuru mkuu wa wilaya ya makete mhe Kissa Kasongwa pamoja na wananchi kwa kuungana pamoja katika kuweka mazingira safi kwa kuwa kata ya  iwawa ni sehemu ambayo inapokea viongozi wengi hivyo ni jukumu la  kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ili kuweza kuvutia wageni wanapokuja kutembelea wilaya ya makete

Cue…..sauti ya diwani mahenge

mkuu wa wilaya akizungumza na wananchi baada ya usafi

Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa taka na usafi wa mazingira Omari Khamis amesema kuwa kuwa leo ni siku ya usafishaji duniani ambayo ilitangazwa pia na umoja wa mataifa  (UN) hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuweza kuhakikisha mazingira yanakuwa safi huku diwani viti maalumu Anifa sanga akiwashukuru  wananchi kwa kujitokeza kwenye zoezi hilo la usafi

Cue……sauti ya khamis vs anifa

Nae mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa ndg Joseph mbilinyi amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi  kwenye shughuli ya usafi huku akiwasisitiza kuwa zoezi hilo la usafi  linatakiwa kuwa endelevu na hata kwenye makazi yao ya kila siku

Cue…………sauti ya joseph mbilinyi

dc makete azungumza na wananchi

Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi la usafi  akiwemo imelda sanga wamepongeza kwa jitihada hizo za kuhakikisha mji wa iwawa unakuwa safi huku wakiwataka wananchi kuacha tabia ya kutupa pampas kwenye mitaro ya mifereji kwakuwa inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kuweza kutokea

Cue…………sauti ya wananchi

wananchi wakimsikiliza dc makete baada ya kumaliza shughuli ya usafi

Siku ya Usafi Duniani ilianzishwa mwaka 2023 na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama siku ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Septemba ambapo kwa wilaya ya makete imeadhimishwa hii leo septemba 19,2026