Wananchi pimeni Ardhi mpate Hatimiliki-Maofisa Ardhi Makete
Kitulo FM

Faida za hatimiliki

September 1, 2023, 7:25 am

Idara ya Ardhi wilaya ya Makete imewasihi wananchi kujitokeza kupimiwa ardhi ili waweze kupata hatimiliki za ardhi.

Akizunguzungumza na Kitulo FM Ibrahim Wawa Afisa Ardhi na Mipango Miji halmashauri ya wilaya ya Makete amesema ili kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiwasumbua wananchi wengi ni vema sasa wakamiliki ardhi yao kwa kuwa na hatimiliki.

Akijibu maswali ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali, mkuu wa Idara ya Ardhi Ndg. Edward Mwaigombe kuhusu umilikishwaji wa ardhi kimila amesema zipo taratibu zinazofuatwa kuhusu umilikishwaji wa ardhi kwa watoto na ndugu.