Kitulo FM
Kitulo FM
11 June 2026, 9:41 am

Wananchi wakitoa hoja zao kwenye mkutano wa kijiji mbele ya mkurugenzi
kutokana na wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu wananchi wameishukuru serikali kwa kutoa pesa itakayo saidia ujenzi mpaya wa shule ya sekondari katika kata ya Mlondwe, Makete
na mwandishi wetu
Wakazi wa Kijiji cha Ng’onde , kilichopo kata ya Mlondwe, Halmashauri ya Wilaya ya Makete, wameishukuru serikali kwa kuwapa Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 583,180,028.00 za Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Kata, ambayo itaenda kuwa Mkombozi wa Upatikanaji wa Elimu katika Kata hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya makete akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ng’onde
Hayo yamebainishwa leo mara Baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Jerry Daimon Mwaga, kukagua eneo ambalo litatumika katika Ujenzi wa Shule hiyo ya Sekondari ya Kata ya Mlondwe ambapo wananchi hao wameonyesha kufurahishwa na ujio wa shule hiyo katika eneo hilo kwakuwa ilikuwa ndoto yao kwa mda mrefu.

Wakazi wa kijiji cha Ng’onde wakiwa kwenye mkutano na mkurugenzi
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Jerry Daimon Mwaga, amesihi wananchi ha, kutoa ushirikiano wa Kutosha katika Ujenzi w Shule hiyo ya Sekondari, sambamba na kuomba zabuni mbalimbali katika mradi huo kwakuwa uwepo wake kwao ni fursa tosha ya kiuchumi.