Kitulo FM

Miti ya matunda yapandwa kupunguza udumavu wilayani Makete

October 10, 2023, 4:14 pm

Mkuu wa wilaya Makete Mhe:Sweda akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Makete Ndg:William Makufwe pamoja na Balozi wa Mazingira Tanzania.picha na Aldo Sanga

Ikumbukwe kua Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka vipaumbele kwa mwaka 2023/2024 kusimamia utekelezaji wa mpango kabambe wa hifadhi na usimamizi wa mazingira na kuchukua hatua za kupunguza uharibifu wa mazingira

na Aldo Sanga

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan chini ya ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Balozi wa Mazingira nchini Tanzania Ndg. Ahidi Jailosi Sinene amepanda miche ya Matunda ya Parachichi katika eneo la Ofisi za Chama cha Mapinduzi pamoja na Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la Upandaji miti, Balozi Sinene amesema kuwa, serikali imetia juhudi katika utunzaji wa mazingira kwa lengo la kuokoa viumbe hai, pamoja na ustawi wa maeneo, hivyo miti ya matunda iwe chachu kwa jamii ili kuondokana na udumavu

sauti ya balozi wa mazingira Tanzania Ahidi Sinene

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda, ameishukuru serikali kupitia kwa Balozi Sinene, kwa kutembelea wilaya ya Makete, na kufanya uhamasishaji katika utunzaji wa mazingira, huku akitoa rai kwa wananchi kuepuka uchomaji wa moto holela.

sauti ya Mkuu wa Wilaya Makete Mhe,Sweda

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg. William M. Makufwe amesema kuwa, wilaya hii inafursa nyingi za kibiashara ikiwemo kilimo cha viazi na uzalishaji wa mazao ya Misitu, ambapo amewasihi wananchi kuachangamkia fursa hiyo na kuacha kuharibu mazingira.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauli ya wilaya Ndg,William Makufwe

Ikumbukwe kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka vipaumbele kwa mwaka wa 2023/2024 kusimamia utekelezaji wa mpango kabambe wa uhifadhi na usimamizi wa mazingira na kuchukua hatua za kupunguza uharibifu wa mazingira hapa nchini

viongozi wa Wilaya ya Makete DED kushoto na DC Samweli Sweda wakiwa na Balozi wa mazingira Tanzania Ahidi Sinene wakiuandaa Mche wa Parachichi.picha na Aldo sanga
Viongozi wa CCM Wilaya ya Makete Katibu wa UVCCM Hassan Kapolo Na Katibu Itikadi Na Uenezi kata ya Isaplano Lauphodi Michaeli (Mackfod) wakiwa na balozi wa mazingira Tanzania Ahidi Sinene Wakipanda mche wa mparachichi.picha na Aldo Sanga