Miradi itekelezwe kwa haraka
Kitulo FM

DED Makete: Ujenzi sekondari Mwakavuta ukamilike kabla ya Agosti 2023

June 13, 2023, 8:23 am

MIRADI IENDE HARAKA TUNAJIANDAA KUPOKEA WANAFUNZI MWEZI AGOSTI 2023 -DED MAKETE

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe ameitaka kamati ya ujenzi shule ya sekondari Mwakavuta pamoja na uongozi wa shule kwa kushirikiana na ofisi ya ujenzi na manunuzi halmashauri ya wilaya ya Makete kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema kama walivyopanga.

Shule ya sekondari Mwakavuta iliyopo kata ya Iniho imepokea shilingi milioni 773 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 9, bweni 4 na vyoo matundu 14 huku ikitarajia kupokea wanafunzi kidato cha 5 wasiopungua 789 ifikapo Agosti 13, 2023.

Zaidi tembelea website yetu ya maketedc.go.tz, Instagram Kitulofmtz na YouTube Makete Account