Kitulo FM
Kitulo FM
22 July 2026, 10:04 am

viongozi wa kijiji wakiwa pamoja na diwani wa kata ya tandala kwenye mkutano wa kijiji
licha ya baadhi ya wananchi kupatiwa mafunzo ya kutumia bunduki wananchi wameiomba serikali kuwapa bunduki na risasi kwa lengo la kufukuza ngedere waharibifu wanaoharibu mazao yao shambani na kukosa mazao mengi ambayo walitarajia kuyapata na imekuwa ikiwaletea adha kubwa wakulima hao
na mwandishi wetu.
Kutokana na uharibifu wa mazao wanaoupata kutokana na uwepo wa ngedere, wananchi wa Kijiji cha Ihela wilayani Makete mkoani Njombe wameomba wananchi waliopewa mafunzo ya kutumia bunduki, wapewe bunduki na risasi wazitumie kufukuza wanyama hao
Wananchi hao wametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kijiji hicho wakati diwani wa kata ya tandala mhe ignatio mtawa alipokuwa akifanya ziara kijiji kwa kijiji kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi
sauti za wananchi ihela
kulingana na ombi hilo la wananchi wa ihela Afisa Kilimo Kata ya Tandala Bruno Mhitche akatolea ufafanuzi jambo hilo akisema zoezi hilo ni la kutishia wanyama na si kuwaua, na pia utaratibu kwa sasa umebadilika
sauti ya afisa kilimo bruno
Naye diwani wa kata ya Tandala Egnatio Mtawa amewaeleza wananchi kuwa umiliki wa silaha sio jambo rahisi kama wanavyofikiri, na kwamba sheria za nchi kuhusu umiliki wa silaha zipo pale pale.
sauti ya diwani mtawa