Kitulo FM

Ujenzi Kituo cha Afya Lupalilo, DC ahimiza Usimamizi

January 18, 2023, 11:07 am

 

Mwonekano wa Kituo cha Kituo cha Afya Lupalilo

Ujenzi wa Kituo cha Afya Lupalilo awamu ya pili umefikia hatua nzuri baada ya kuwa katika hatua za mwisho wa ujenzi.

Kituo hicho ujenzi wake ulianza kwa wananchi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje na Serikali ikaunga mkono kwa kutoa Milioni 250 awamu ya kwanza na awamu ya pili Milioni 250 na kufanya jumla ya Milioni 500 kujenga Kituo hicho mpaka kukamilika.

 

Mkuu wa Wilaya Mhe. Juma Sweda (mwenye kofia) akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Lupalilo

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amefika eneo la Mradi na kukagua utekelezaji wake huku akimtaka Mtendaji wa Kata ya Lupalilo kusimamia ujenzi huo kikamilifu ili Kituo kikamilike.

Mhe. Sweda amesema Mtendaji anapaswa kusimamia mafunzi kwa karibu kwa ushirikiano na Kamati ya Ujenzi ili kuharakisha umaliziaji wa Tiles na kupiga rangi ndani ya vyumba vinavyojengwa, ufungaji wa Milango pamoja na kufanya baadhi ya marekebisho kwenye mfumo wa Umeme.