Mkurugenzi wa Elimu na Vijana Mwl. Kudra Jekela akizungumzia kuhusu kongamano hilo
Kitulo FM

Vijana kufanya kongamano Makete

June 23, 2023, 7:57 am

Mkurugenzi wa Elimu na vijana KKKT-DKK Makete Mwl. Kudra Jekela akizungumza na WanaMakete hususani Wakristo na Vijana wote kupitia Redio Jamii (KITULO FM) kuhamasisha wajitokeze kwa wingi kwenye Kongamano la Vijana linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Juni-02 Julai 2023.

Kudra amesema Kanisa linakusudia kuwanufaisha Vijana kujibu maswali ya Maisha yao Kiuchumi, Kijamii na Kiroho hivyo Kanisa ni Sehemu ya Majibu hayo kwa Kijana wa sasa na baadaye

Ameongeza kuwa Kongamano hilo litahusisha vijana kufundishwa neno la Mungu, Uchumi, Urafiki na uchumba, Michezo mbalimbali na zawadi zitatolewa kwa washindi

Kongamano hilo litafanyika Makete Mjini kuanzia tarehe 30 Juni hadi 02 Julai 2023