Kitulo FM
Kitulo FM
17 June 2026, 6:31 am

Wito umeendelea kutolewa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika kuendelea kulindwa kwa watoto dhidi ya vitendo viovu ili kuwa na taifa bora la hapo baadae
Na mwandishi wetu
Wakazi wa Wilaya ya Makete, mkoani Njombe, leo June 16,2026, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanazingatia malezi bora kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kujenga jamii yenye uelewa kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Hayo yamebainishwa na Afisa Tawala, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Makete, Ndg. Onesphoria Ngogo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Kissa Kasongwa, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ,ambayo kiwilaya yamefanyika katika Kijiji cha Ivalalila Kata ya Iwawa.
Aidha, Ndg. Ngogo, ameongeza kuwa ulinzi wa afya na mazingira bora ya kujifunzia ndio msingi wa kufaulu kwa mtoto na mzalendo kwa Taifa lake la Tanzania, sambamba na kuzuia watoto kutoendeleza matumizi ya mitandao ya kijamii kwakuwa imekuwa na madhara katika ukuaji wao.
Ngogo amesema kuwa licha ya vitendo vya kikatili ambavyo watoto wamekuwa wakifanyiwa serikali bado imekuwa ikifanya jitihada za kuhakikisha wanaotenda vitendo viovu dhidi ya watoto wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria
Afisa tawala ngogo

Watoto wakiendelea kutumbuiza kwenye aadhimisho ya mtoto wa Afrika
Akisoma risala kwaniaba ya wanafunzi wa wilaya ya makete Esta Mwihava kutoka shule ya msingi iwawa amesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan pamoja na Halmashauri ya Makete kwa jitihada wanazozifanya za kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa,watoto kupelekwa shule bila kubaguliwa pamoja na kutatuliwa kwa changamoto ikiwemo ukatili
Risala…….watoto 01

Viongozi wakiwa jukwaa kuu wakiimba wimbo wa taifa la Tanzania
AIDHA amebainisha baadhi ya changamoto wanazopitia kama watoto ikiwemo mimba za utotoni,utoro kwa wanafunzi, wazazi kutotimiza mahitaji ya watoto kwa wakati huku wakiiomba hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya baadhi ya watu wanaofanya matendo ambayo ni kinyume na maadili ili kuweza kufanikisha mtoto anatimiza ndoto zake
Risala watoto 02
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mh Rabson Mahenge amewataka wananchi wa Makete kuhakikisha wanalinda na kudumisha haki za watoto kwa vitendo, na sio kwa maneno kwakuwa mustakabali wa taifa upo mikononi mwa watoto, hivyo ni jukumu la pamoja kuwapatia elimu bora, afya na mazingira salama.
Sauti ya diwani mahenge

Wazazi na wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya mtoto wa afrika
Edward Leornad ambaye ni mtendaji wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya makete amewataka wazazi kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili huku akiwasii kushirikiana kwa pamoja katika kufuatilia mienendo ya watoto wao
Sauti ya askali Edward
Nae Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa ndg Joseph Mbilinyi amewasihi wazazi na walezi kuwatunza watoto wao vyema ili wakuwe katika maadili yaliyo mema huku akiwashukuru wananchi wa ivalalila kwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo
Mwenyekiti Joseph Mbilinyi
Ikumbukwe kuwa, siku hii inasherekewa kila mwaka ifikapo juni 6 tangu mwaka 1991, ilipoteuliwa na na umoja wa afrika katika kuenzi michango ya watoto walioshiriki katika maandamano mji wa Soweto 1976, pamoja na kujenga jamii yenye uelewa juu ya umuhimu wa elimu bora kwa watoto
Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo mtoto ni malezi msingi wa familia bora kwa taifa imara