Kitulo FM

wakulima wahimizwa kuhuisha taarifa zao kwenye daftari la wakulima

September 12, 2023, 10:29 am

Mtaalamu kutoka Idara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Makete Ahmed Kichombaki.picha na furahisha nundu

kulingana na serikali kutoa ruzuku ya pembejeo wakulima wametakiwa kuendelea kuhuisha taarifa zao kwenye daftari kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kupata pembejeo

na mwandishi wetu

Wakulima Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kwenda kwenye Ofisi za Vijiji ili kuhuisha taarifa zao kwenye Daftari la wakulima

amesema kwa msimu wa kilimo 2023/24 wakulima wameanza kuandikishwa kwenye daftari la wakulima ili waweze kupata pembejeo za kilimo kwa bei ya ruzuku

Akizungumza na Kitulo FM Leo Septemba 5, 2023 Mtaalamu kutoka Idara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Makete Ahmed Kichombaki amesema kwa msimu wa kilimo 2023/24 wakulima wameanza kuandikishwa kwenye daftari la wakulima ili waweze kupata pembejeo za kilimo kwa bei ya ruzuku

sauti ya Mtaalamu kutoka Idara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Makete Ahmed Kichombaki

Kichombaki ameelezea changamoto ya wakulima kuwa na mwitikio mdogo wa kujiandikisha na kuwasihi wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha zoezi hilo

sauti ya Mtaalamu kutoka Idara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Makete Ahmed Kichombaki

Afisa Takwimu na pembejeo Wilaya ya Makete Ndg. Mnyama Charles amesema dirisha la usajili lilianza Septemba mosi na linatarajiwa kufungwa tarehe 15 Septemba, 2023

sauti ya Afisa Takwimu na pembejeo Wilaya ya Makete Ndg. Mnyama Charles

Msimu wa kilimo 2023/24 umeanza wilayani makete ambapo wakulima wamekuwa wakinufaika na pembejeo za ruzuku kutoka serikali kwa bei ya punguzo kutoka laki moja na nusu hadi elfu sabini.