Kitulo FM
Kitulo FM
12 June 2026, 6:20 pm

Watumishi wa hospitali ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wamepongezwa kwa utoaji wa huduma bora kwa wananchi wanapofika kwa ajili ya kupata huduma na kuwasisitiza kuendelea kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Na Omben Mgongolwa
Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, leo ametembelea na kuona wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Makete, ikiwa ni pamoja na kujionea hali ya utoaji huduma.
Mhe. Kasongwa mara ya kuwatembelea wagonjwa, amewapongeza watumishi wa Hospitali hiyo kwa kutimiza majukumu yao kikamilifu na kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Aidha, Mhe. Kissa Kasongwa, amewasihi watumishi hao kuendelea kutoa huduma Bora kwa wagonjwa kwakuwa Serikali imewaamini, na imekuwa ikiendelea kuboresha utolewaji wa huduma za Afya ndani ya Wilaya ya Makete kwa kujenga miundombinu ya kisasa.

Kwa Upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Makete, Dkt. Ligobert Kalisa, amesema ziara ya Mkuu wa Wilaya Hospitalini hapo imeongeza hamasa katika utendaji kazi pamoja na kutambua umuhimu wa kada hiyo katika kuhakikisha Afya za wananchi zinaimarika.