Kitulo FM

Wananchi waiomba Serikali kujenga Barabara Kigulu

January 16, 2023, 7:46 am

 

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda akizungumza na wananchi wa Kigulu

Wananchi wa Kijiji cha Kigulu wameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kijiji hicho ili kurahisisha shughuli za usafiri na kuongeza mzunguko wa Uchumi kwa wananchi.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda wananchi hao wamesema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa kwa wananchi hao ni ukosefu wa Barabara ya Itunge mpaka kufika kijijini hapo.

Wakati huohuo wananchi hao wametumia fursa hiyo kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda kufika kijijini hapo na kusikiliza changamoto zao pamoja na kukagua miradi ya zaidi ya Milioni 100 inayotekelezwa katika kijiji hicho, Pia wamempongeza Mbunge na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi hiyo

Kwa upande wake Diwani Kata ya Kigulu Mhe. Simeon Mwaikenda amesema changamoto kubwa inayowakabili wananchi wake ni kukosekana kwa barabara ya uhakika

Mkuu wa Wilaya ya Makete amesema wananchi hao kutokuwa na barabara ni hatari hususani wanapopatwa na shida ya wagonjwa hulazimika kusafirisha kwa machela, hivyo atahakikisha Serikali inawasaidia wananchi hao

Wananchi wa Kijiji cha Kigulu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Makete alipofika kuzungumza na kusikiliza kero zao kwenye kijiji hicho