Wananchi wa mbarali, Spika wa Bunge na Mbunge Jimbo la Makete wakiwa Ibadani kumuaga Marehemu Francis
Kitulo FM

Mbarali wamlilia Mtega

July 5, 2023, 7:16 am

Mbunge wa Makete Mh.Festo Sanga ameungana na Wanambarali hii leo kwenye ibada maalum ya kumuaga aliyekuwa mbunge wa Mbarali marehemu Francis Mtega aliyepatwa na umauti baada ya kupata ajali akitokea shambani kwake huko huko Mbarali-Mbeya.

Ibada hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackon, Wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa pamoja na wananchi wa Mbarali.