Shirikisho la watu wenye ulemavu Makete wapata viongozi
Kitulo FM

Walemavu Makete wafanya Uchaguzi

August 31, 2023, 9:19 am

Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Wilayani Makete limefanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Chama hicho na kumchagua BI. MARIA MSIGWA kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo

 Katika uchaguzi uliofanyika Agosti 30, 2023 katika ukumbi mdogo wa mikutano wa  halmashauri ya wilaya ya makete wajumbe waliokuwa na sifa za kupiga kura walikuwa 12 ambapo BI. MARIA MSIGWA amepata kura 7 za ndio huku mpinzani wake katika kinyanyanyiro hicho Noadi Tweve akipata kula 5

Akizungumza mara baada ya uchagauzi huo Mwenyekiti wa Shirikisho hilo BI. MARIA MSIGWA amesema atasharikiana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete katika kuwafichua walemavu na kuwasaidia kupata haki zao

Aidha amesema kuna baadhi ya familia zinawaficha watu wenye ulemavu na wengine wamekuwa na tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu jamba ambalo si nzuri na kusisitiza kuwa mtu mwenye ulemavu anahaki sawa na mtu mwingine kwa mujibu wa katiba ya jamuhuli ya muungano wa tanzania

Katika uchaguzi huo pia Saimoni Mahenge amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti washirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Wilaya ya  Makete  kwa kupata kula 12 za ndio.

Tumwanuke Mahenge amechaguliwa kuwa Katibu shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya  makete kwa kupata kura 8 za ndio na kura 4 za hapana

Huku Stella Mahenge akichaguliwa kuwa mtunza fedha wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya  makete akipata Kura 12 za ndio.