Mwenyekiti wa Kitongoji akikabidhiwa Bendera nyekundu inayoaashiria uchafu na alama ya hatari katika Kitongoji chake
Kitulo FM

Mwenyekiti wa kitongoji akabidhiwa bendera nyekundu kitongoji chake kuwa kichafu

June 23, 2023, 7:40 am

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kilambo Kijiji cha Ujuni Ndg. George Mwasanga amekabidhiwa bendera nyekundu kama alama ya kitongoji chake kuwa na Mazingira yasiyoridhisha kwa usafi.

Kupitia Kikao cha Kamati ya Maendeleo Kata ya Kitulo kilichofanyika tarehe 21 Juni 2023 katika kutekeleza mpango kazi wao waliojiwekea kuhusu vyoo, makazi bora na usafi wa Mazingira uliopitishwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23 kila Kaya ni lazima kuwa na choo bora, nyumba bora na usafi wa jumla wa Mazingira.

Katika kutekeleza mpango kazi huo jana Mwenyekiti wa kitongoji cha Kilambo Kijiji cha Ujuni baada ya ukaguzi huo Kitongoji chake kimekutwa na hali isiyoridhisha ya usafi na kutokuwa na vyoo bora na nyumba nyingi za mabanzi

Hivyo Kikao kimemkabidhi bendera nyekundu Mwenyekiti huyo mbele ya wajumbe wa KAMAKA ikiwa ni ishara ya usimamizi mbovu wa mpango kazi waliojiwekea.

Kwa mantiki hiyo bendera hiyo itakaa ofisini kwa Mwenyekiti wa Kitongoji huyo mpaka pale atakaporekebisha mapungufu yaliyokutwa kwenye Kitongoji chake.