Wanaume washauriwa kwenda kwa Wataalamu tatizo la Nguvu za Kiume
Kitulo FM

Wanaume washauriwa kuona wataalam tatizo nguvu za kiume

June 8, 2023, 10:23 am

Wanaume wametakiwa kufuata ushauri wa wataalum wa afya pale ambapo wanataka kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ili waweze kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa matumizi ya dawa hizo.

Akizungumza na Kitulo FM, mkaguzi wa dawa na vifaa tiba kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba nchini Tanzania (TMDA) Bi. Grace kapande amesema kumekuwa na wanaume wengi wanaotumia dawa za kuongeza nguvu za kiume pasipo kufuata utaratibu na kutokujua tatizo.

Amesema dawa za kuongeza nguvu za kiume ni lazima mtumiaji awe amegundulika ana tatizo hilo na daktari atamshauri dawa ambayo anatakiwa kuitumia na namna gani ya kuitumia.

Ameongeza kuwa tatizo  la nguvu za kiume sio lazima utumie dawa na kwa mtu mbaye anatakiwa kutumia kutumia dawa hizi ni lazima awe na tatizo kubwa kwani kuna wengine wakitumia chakula kuna uwezekano mkubwa wa kupona.

B. Grace amesema kuna sababu nyingi zinazosababisha upungufu wa nguvu za kiume hivyo ni vema kugundua tatizo kabla ya kuanza kutumia dawa hizo

Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo katika mfumo wa uzazi wa mwanaume yanayopelekea uume kuwa na uwezo mdogo au kutokuwa na uwezo kabisa wa kuhimili tendo la ndoa ambapo kuna aina nne za dawa ambazo mwanaume anaweza kutumia ila tafiti zinaonyesha dawa hizi hazitibu wala kumaliza tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume bali husaidia kutatua tatizo wakati zinapotumika.