Kitulo FM

Askofu Shoo awataka waumini Makete kuungana ujenzi wa kanisa

October 28, 2023, 3:52 pm

Askofu mkuu wa wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick Shoo pamoja na askofu mkuu wa dayosisi ya kusini ya kati wilson sanga kwenye uwekaji wa jiwe la msingi.picha na Rose njinile

Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, unaweza kusema hivyo baada ya wananchi kutoka makete na wadau kutakiwa kuungana katika kufanikisha ujenzi wa hekaru la mwenyezi Mungu.

Na Rose njinile.

Inakadiliwa kuwa jumla ya zaidi ya shilingi bilioni moja zinahitajika katika kukamilisha ujenzi wa kanisa  kuu la dayosisi ya kusini kati makete mjini

Hayo yamesemwa kwenye  zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika kanisa kuu la dayosisi ya kusini kati  zoezi ambalo limefanyika na mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania dkt Fredrick shoo

Akisoma taarifa ya ujenzi huo katibu mkuu wa dayosisi ya kusini kati mch Ezekiel Sanga amesema kuwa kutokana na changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo katika kufanikisha ujenzi huo unakamilika mpaka sasa mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 400

sauti ya katibu mkuu wa dayosisi kusini kati Ezekiel Sanga

Muonekano wa ujenzi wa kanisa jipya la dayosisi ya kusini kati Makete mjini

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi askofu mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrik shoo amewataka wanamakete kuungana katika kufanikisha zoezi hilo la ujenzi Unakamilika

Sauti ya mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick Shoo

Nae askofu mkuu wa KKKM  kutoka nchi jirani ya Malawi  MSUKU ambaye nae alikuwa katika zoezi hilo ameipongeza serikali kwa maendelo yanayofanyika katika wilaya ya makete pamoja na maendeleo ya kujenga hekaru la mungu

sauti ya askofu kutoka nchi ya malawi Msuku

Baadhi ya Maaskofu wakiwa na mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick Shoo kwenye uwekaji jiwe la msingi

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya makete mh juma sweda amewaomba wanamakete kushirikiana katika kufanikisha ujenzi wa kanisa hilo huku akimshukuru baba  askofu Fredrick shoo kufika makete

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Makete mh Juma Sweda

Aidha nao baadhi ya washirika waliofika katika kushuhudia zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi akiwemo aida chengula wamempongeza mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Fredrick shoo kufika na kufanikisha zoezi hilo huku wakiwataka wanamakete walioko nje ya makete kuweza kufanikisha zoezi la ujenzi linakamilika

Suati ya washiriki wa kanisa la lutherani dayosisi ya kusini kati

Hata hivyo zoezi hilo la uwekaji jiwe la msingi kanisa kuu la dayosisi ya kusini kati umeshuhudiwa na baadhi ya waumini wa kanisa hilo