Mkakati wa kuendeleza Kilimo cha Ngano Makete
Kitulo FM

Mkuu wa Mkoa wa Njombe awapongeza watumishi Makete kwa Ubunifu

March 7, 2023, 9:35 pm

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na watalaamu kutoka SUA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka amewapongeza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa ubunifu wa Miradi mbalimbali ikiwemo Kilimo cha zao la Ngano.

Pongezi hizo amezitoa leo Machi 7, 2023 akiwa kwenye Kikao kazi kati ya Maafisa Ugani na Kilimo sambamba na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA.

Mhe. Mtaka amesema ubunifu wa Miradi unaofanywa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ni wa Kipekee ukilinganisha na uhalisia wa Ukusanyaji Mapato ambao pia umeendelea kuongezeka kila siku.

Sauti………….Mtaka Habari

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Wiliam Makufwe amesema Halmashauri imetenga zaidi ya shilingi Milioni 200 kwa wa fedha ujao 2023/24 kwa ajili ya Mkakati wa kuongeza tija ya uzalishaji wa zao la Ngano Makete.

Sauti……………….Makufwe

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete

Kwa upande wao Wanafunzi Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA Morogoro wameshukuru mapokeo waliyopata kutoka Halmashauri ya Wilaya Makete na kuahidi kuwasaidia wakulima na kuleta mabadiliko yenye tija katika zao la Ngano Wilayani Makete.

Sauti………………Watalaamu

Wataalamu kutoka Chuo cha SUA