Kitulo FM

Zaidi ya kaya 20 zaathiriwa na upepo mkali Makete

January 20, 2024, 9:01 pm

Moja kati ya makazi ya waathirika kulia ni Dc Makete Mh:Juma Sweda aliyevaa kofia yenye rangi ya bendera ya Taifa picha na mwandishi wetu

Ikiwa mamlaka za utabiri wa hali ya hewa nchini zinazidi kutoa tahadhari juu ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini, baadhi ya maeneo katika mikoa na wilaya kumetokea athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na vifo vya binadamu pamoja na uharibifu wa miundombinu.

Na mwandishi wetu

Mvua iliyoambatana na upepo mkali jioni ya tarehe 19/1/2024 imesababisha zaidi ya kaya 20 kukosa makazi kwa kuezua bati za nyumba na zingine kubomoka katika kata ya Luwumbu, Lupalilo na Mang’oto wilayani Makete mkoani Njombe.
Taasisi kadhaa pia zimekumbwa na maafa hayo ikiwemo kanisa la TAG Luwumbu, kanisa la TAG Ipululu, Ofisi ya chuo Cha Mategemeo Mang’oto na vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Mango’to
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amefika maeneo yaliyopatwa na maafa hayo kuwapa pole na kuwapongeza.Wanajamii kwa ushirikiano walioutoa kwa wenzao walioezuliwa nyumba zao huku akihamasisha kupanda miti ili kuzuia athari zinatokanazo na mvua inayoambatana na upepo
Diwani Kata ya Luwumbu Mhe. Felix Kyando amesema wananchi wake wameanza kusaidia kupiga bati baadhi ya nyumba zilizoezuliwa na kukusanya michango Iii kununua bati na vifaa vya kusaidia ujenzi Ili nyumba ambazo zinahitaji ukarabati mkubwa ziweze kurekebishwa huku akiiomba Serikali kuwasaidia pale walipokwama
Kamati ya maafa Wilaya itaenda maeneo yote yaliyopata maafa Ili kutathimi hasara iliyojitokeza ili Serikali iweze kuwasaidia wananchi warudi katika maisha yao ya kila siku