Kitulo FM
Kitulo FM
3 March 2023, 2:42 pm
Idara ya Afya Wilaya ya Makete Kitengo cha Lishe imeendelea kutoa Elimu ya Afya na Lishe kwa wanawake vijiji Mbalimbali Wilayani Makete.
Elimu hiyo ni kuhusu Lishe bora kwa watoto kuanzia miezi 6 na kuhakikisha wananyonyesha Maziwa halisi ya Mama kwa mtoto aliyechini ya Miezi 6.
Jackline Nanauka Afisa Lishe Wilaya ya Makete akiwa kijiji cha Ivalalila amezungumza na wanawake wenye watoto walipohudhuria mafunzo hayo yenye lengo la kutoa elimu ya Afya na Lishe amewasihi kuzingatia maelekezi yanayotolewa na wataalamu mara kwa mara
