Kitulo FM

Wazazi acheni kuwapa simu watoto wenu

22 June 2026, 7:34 pm

Afisa tawala wilaya ya makete ndg  Onespholia Ngogo

kutokana na wimbi la watoto kutumia simu wito umetolewa kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuacha tabia hiyo ya kuwazoesha watoto simu ili kuwa na kizazi kilicho bora pamoja na kuacha kuwalaza watoto na watu wengine ili kuepukana na vitendo vya kikatili

na mwandishi wetu

Wito umetolewa kwa wazazi wilayani makete mkoni njombe kuacha tabia ya kuwapa simu watoto wao jambo ambalo linaweza kupelekea  watoto hao kujifunza au kuangalia vitu ambavyo sivyo  

Hayo yamesemwa na Afisa tawala wilaya ya makete ndg  Onespholia Ngogo alipokuwa akizungumza na wananchi wa ivalalila kata ya iwawa  ambapo amesema kuwa simu zimekuwa zikipelekea mazingira mabaya au kushuka kwa mmomonyoko wa maadili dhidi ya watoto wao

afisa tawala 01

mtendaji wa dawati la jinsia na watoto makete afande Edward Leaornad

kwa upande wake mtendaji wa dawati la jinsia na watoto makete afande Edward Leaornad amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na baadhi ya ndugu kwa kigezo shetani amewapitia na kuwataka wazazi kuacha tabia ya kuwalaza watoto na watu wazima ili kuepusha vitendo vya kikatili ambavyo vinaweza kujitokeza

 edward 01

Aidha kutokana na baadhi ya watoto kujikita katika michezo isiyofaa ambayo ni kinyume na maadili Afande Edward amewataka  wazazi na jamii kwa ujumla  kuendelea kufuatilia maendeleo na michezo ya watoto ili kuwa na kizazi bora

afande 02