Kitulo FM

Mchungaji wa kwanza Makete atunukiwa shahada ya juu ya heshima

October 18, 2023, 12:46 am

Mwakilishi wa Dkt. Tupevilwe Lugavano Sanga baada ya kupokea Shahada ya Juu ya Heshima.na mwandishi wetu

Chuo Kikuu cha Iringa kimemtunuku Shahada ya Juu ya Heshima Hayati Mchungaji Dkt. Tupevilwe Lugano Sanga.

Mchungaji Tupevilwe Lugavano Sanga aliyezaliwa 1898, ni Mchungaji wa mwanzoni kabisa katika jamii ya Wakinga aliyetoa maisha yake kumtumikia Mungu pamoja na kuhamasisha maendeleo ya kiroho na kijamii katika jamii ya Wakinga kwa kushirikiana na Shirika la Wamisionari wa Trump Berlin.

Akizungumza katika Mahafali Maalum, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Jenerali Venance Mabeyo amesema, shahada hii ya heshima imetolewa ikiwa ni kutambua na kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na mchungaji Tupevilwe Sanga ikiwemo ujenzi wa shule, vituo vya afya pamoja na kuhamasisha upatikanaji wa eneo la kujengwa hospitali ya Consolata Ikonda.

mkuu wa chuo cha Iringa Jenerali Venance Mabeyo akimkabidha Shahada ya Juu ya heshima mwakilishi wa hayati Tupevilwe Sanga
mkuu wa chuo cha Iringa Jenerali Venance Mabeyo akimkabidha Shahada ya Juu ya heshima mwakilishi wa hayati Tupevilwe Sanga
Baba askofu Willisoni Sanga kiwa na mwakilishi kutoka uholanzi wakionyesha nakala za Shahada ya Juu ya Heshima ya Tupevilwe Sanga Baada ya kukabudhiwa na Mkuu wa Chuo kikuu cha Iringa

Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka katika mahafali hayo, alitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Njombe na Mkurugenzi kuhakikisha Hayati Mchungaji Tupevilwe anakumbukwa kwa shule mojawapo Wilayani Makete kuitwa jina lake, maagizo ambayo yalitekelezwa papo hapo na kutangazwa kwa shule mojawapo ya Sekondari iliyo kwenye ujenzi kupewa jina la Mchng. Dkt. Tupevilwe Lugavano Sanga

Huu ni muendelezo kwa Chuo Kikuu cha Iringa kutoa shahada ya juu ya Heshima kwa kuwatambua watu mbali mbali wenye mchango katika jamii.