Wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya Maskini Kijiji cha Ivilikinge waeleza mafanikio ya mradi huo na kuishukuru Serikali kwa kuwasaidia wazee
Kitulo FM

Wanufaika TASAF Makete waishukuru serikali

June 27, 2023, 4:50 pm

Wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya maskini kijiji cha Ivilikinge waeleza mafanikio ya mradi huo na kuishukuru serikali kwa kuwasaidia wazee.

Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wanufaika, wamesema mradi huo umebadilisha hali zao kiuchumi na kuwafanya wengine kujihusisha na kilimo cha Viazi na Parachichi.

Tolemwimehe Tweve mnufaika na Upendo Tweve msaidizi wa mnufaika wa TASAF wamesema wamefanikiwa kujihusisha na kilimo cha zao la viazi, ufugaji wa kuku, nguruwe na hata mbuzi huku wakielezea mafanikio ya mradi huo.

Estini Tweve mkazi wa kijiji cha Ivilikinge amesema serikali imefanya kazi kubwa ya kubadilisha hali za kiuchumi kwa wanufaika wa mradi huo na jamii inashuhudia mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi hao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ivilikinge Cosmasi Luvanda amewapongeza wananchi wake hususani wanufaika wa maradi wa TASAF kwa kujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji jambo ambalo baada ya miaka kadhaa mbele wataona mafanikio yake.