Kitulo FM

Jeshi la akiba Makete latakiwa kuimarisha ulinzi na usalama

November 7, 2023, 2:19 pm

Vijana wa jeshi la akiba kata ya Mfumbi wakiwa katika gwalide siku ya kufuzu mafunzo picha na mwandishi wetu

Katika kudumisha uzalendo kwa wananchi wa Tanzania, vijana 99 wa kata ya Mfumbi wamefuzu mafunzo ya jeshi la akiba maarufu kama mgambo wilayani Makete mkoani Njombe lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi na usalama kwa jamii.

Na mwandishi wetu.

Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Samweli Sweda amewapongeza vijana wa kata ya Mfumbi ambao wamehitim mafunzo ya Jeshi la akiba na kuwataka kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika eneo lao wakati wote

Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Samweli Sweda akiwa na kamati ya ulinzi na usalama katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya Jeshi la akiba kata ya Mfumbi picha na mwandishi wetu

Akizungumza na Vijana hao waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la akiba Mhe:Sweda amesema kutokana na kata hiyo kupitiwa na barabara kuu ya Mbeya -Dar es salaam kumekua na mwingiliano wa wageni kutoka sehemu mbalimbali wanaohitaji huduma katika kata hiyo hivyo kuwataka waimalishe ulinzi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu

Jumla ya vijana 99 wamahitimu mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) baada ya kufuzu mafunzo ya kijeshi kwa muda wa siku 90 katika kata ya mfumbi iliopo wikayani Makete