Kitulo FM

Wananchi waishukuru serikali kuwafikishia umeme Igolwa Makete

March 1, 2024, 7:22 am

mbunge Mh:Festo Sanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Igolwa

katika kutekeleza miradi ya umeme vijijini,wananchi wa kijiji cha Igolwa kilichopo katika kata ya Ipepo waipongeza Serkali kwa kuwafikishia Umeme,huku wakiomba Serkali kutatua changamoto ya Barabara.

Wananchi wa kijiji cha Igolwa Kata ya Ipepo Wilayani Makete wameipongeza Serikali na Viongozi wote hususani Mbunge Jimbo la Makete kwa kuwasaidia katika shughuli mbalimbali ikiwemo miradi inayotekelezwa Kijijini hapo.

Pongezi hizo wamezitoa leo Feb 27,2024 wakati Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga alipofika kufuatilia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Kijiji hicho

wananchi wakimsikiliza Mbunge Mh:Festo Sanga

Wananchi wameshukuru kwa kupata Umeme ambapo wamesema hawakujua kama ipo siku Kijiji hicho kitakuja kuwa na Umeme, huku wakiiomba Serikali kuona umuhimu wa Barabara ambayo imekuwa kilio kikubwa kwao na kushindwa kufanya shughuli za Kiuchumi

Mh:Sanga akizungumza na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Igolwa