Kitulo FM

Zao la viazi laozea Shambani

October 18, 2021, 1:58 pm

Zao la Viazi kwa wakulima wa Kata ya Kitulo Wilayani Makete huenda likaozea shambani kwa sababu ya kukosekana soko la uhakika la zao hilo

Kwa mujibu wa Wakulima wa Viazi Kata ya Kitulo, wamesema wengi wao wameshindwa kuvuna viazi shambani msimu wa mavuno kwa sababu ya kuporomoka kwa soko lazao hilo

Akizungumza na kitulo fm Diwani wa kata ya Kitulo Mh. Abel Mahenge amesema kwa sasa bei ya viazi   kwa gunia la debe  tano ya viazi inauzwa shilingi elfu tano (5,000) kutoka elfu arobaini na tano (45,000) jambo ambalo linawaumiza wakulima

Diwani kata ya Kitulo

Wakulima wa viazi wameiomba Serikai kutatua changamoto ya soko la viazi kwani wametumia gharama kubwa kwenye kilimo cha zao hilo.

Kwa mwaka wa mavuna 2019-2020 bei ya viazi ilikuwa  kati ya shilingi 40,000 hadi 50,000 kwa gunia lenye kubeba debe tano lakini kwa sasa bei hiyo imeshuka maradufu jambo ambalo wakulima wanasema kwa  mwaka huu wa mavuno kutokana na bei kuwa chini wamepeta hasara kwenye zao hilo.

Kata ya kitulo ni moja ya kata katika Wilaya ya Makete ambayo inazalisha kwa wingi zao la viazi na wananchi wamekuwa  wakitegemea  zao hilo kujikwamua kiuchumi.