Kitulo FM

Serikali yatoa fedha ujenzi wa madarasa

October 5, 2023, 8:52 am

Mwonekano wa majengo ya madarasa yaliyokamilika ujenzi yaliyojengwa na fedha za serikali shule ya sekondari Matamba. Picha na Furahisha Nundu

Kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Matamba serikali imetoa fedha shilingi milioni 700 kutatua changamoto hiyo,

Na mwandishi wetu.

Zaidi ya Shilingi Milioni 700 zimetolewa na Serikali kujenga madarasa, bweni na yoo katika shule ya sekondari Matamba.

Fedha hizo zimetumika kujenga vyumba 8 vya madarasa, bweni 4 na vyoo matundu 13.

Madarasa, vyoo na mabweni matatu yamekamilika kwa fedha za Serikali Kuu huku bweni moja linalojengwa kwa fedha za SEQUIP likiwa hatua ya kupandisha kuta.