Kitulo FM

kibonge wa Yesu kaja kivingine Tanzania

November 12, 2023, 2:04 am

picha ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tz Kibonge wa Yesu picha na Aldo sanga

Mtumishi wa Mungu na mwimbaji wa Nyimbo za Injili Juma Kyando alimaarufu kwa Jina la Kibonge wa Yesu,ameachia Nyimbo mbili usiku wa kuamukia tarehe 11Nov 2023 ikiwa ni siku ya kumbukizi ya Siku yake ya kuzaliwa

na Aldo Sanga

Mwanamuziki nguli wa nyimbo za Injili nchi Tanzania anayefahamika kwa jina la Juma kyando maarufu kama Kibonge wa Yeu ameachia nyimbo mbili zinazokwenda kwa jina la Yesu na kupenda na Shukrani ikiwa ni siku moja tu kabla ya kusherekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake

Akizungumza na kitulo FM ofisini kwake Kibonge wa Yesu ameshukuru watanzania wote kwa ushirikiano wanaompa ikiwa nai pamoja na kusikiliza nyimbo zake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusambaza na kupakua nyimbo kupitia mitandao ya kijamii.

sauti ya kibonge wa Yesu

katika hatua nyingine kibonge wa Yesu ameeleza hatua aliyofikia kwa sasa kuwa imetokana na unyenyekevu mkubwa pamoja na kumuishia Mungu katika Utumishi wake huku akiomba, watanzania  kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake za sanaaa.

Kwaupande wa mashabiki wa Muziki wa Kibonge wa Yesu wameeleza jinsi wanavyotambua mchango wa Kibonge wa Yesu katika kueneza Injili kupitia Muziki huku wakionyesha shauku kubwa ya Mapokezi ya Nyimbo alizoachia rasmi

Akizungumza kwaniaba ya ofisi mtayarishaji wa muziki wa msanii Juma Kyando ambaye ana fahamika kwa jina la mixing dokta ameeleza namana alivyofurahishwa na kazi za sanaa zinazofanywa na Kibonge wa Yesu huku akieleza furaha yake kuhusiana na siku yake ya kuzalia

sauti ya Mixing Dokta mtayarishaji wa muziki

Treacy kyando ni mdogo wake na kibonge wa Yesu ameeleza jinsi familia wanavyo toa ushirikiano wahali na mali katika kuhakikisha kazi za sanaa ya Kibonge wa Yesu ina songa mbele.

sauti ya Treacy Kyando ambaye ni dada wa msanii Kibonge wa Yesu