Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Makete wafanya uchaguzi na kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri
Kitulo FM

Mhe. Fungo Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya Makete

August 26, 2023, 12:56 pm

Diwani Kata ya Iniho Mhe. Christopher Fungo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Kwa kura zote 26 za Madiwani waliohudhuria Kikao cha Baraza Leo Agosti 25, 2023

Mhe. Fungo anachukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Mhe. Francis Chaula kuondolewa kwenye nafasi hiyo kwa kupigiwa kura na Madiwani za kutokuwa na Imani naye miezi kadhaa iliyopita

Pia Baraza la limemchagua Diwani Viti maalum Tarafa ya Ikuwo Mhe. Hawa Kader Kwa awamu nyingine kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kura 25 kati ya 26 zilizopigwa.