Kitulo FM

Wananchi waaswa kuendelea kutunza miradi ya maendeleo

October 22, 2023, 12:35 pm

Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis na viongozi wa halmashauri katika mradi wa shamba la kilimo cha ngano ugabwa.picha na ombeni mgongolwa

Kutokana na fedha kutolewa kwaajili ya kuendeleza miradi katika maeneo mbali mbali kikundi cha tutunze mazingira kijiji cha ugabwa cha endelea kunufaika na shughuli wanazozifanya kama kilimo pamoja na ufugaji.

Na ombeni mgongolwa

Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis Amewataka watanzania, kuhakikisha kuwa wanatunza miradi ikiwa ni pamoja na kuzitumia vizuri fedha za miradi hiyo ambayo zimekuwa zikipelekwa kwenye maeneo yao.

Mhe. Khamis Khamza Khamis amesema hayo October 18/2023, akiwa ziarani Wilayani Makete, katika kijiji cha Ugabwa, wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya Kuhifadhi Ardhi katika bonde la Ziwa Nyasa.

sauti ya Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis

Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis akipewa maelezo na Afisa Mifugo wa Wilaya ya Makete, Ndg. Aldo Mwapinga,

Naye, Afisa Mifugo wa Wilaya ya Makete, Ndg. Aldo Mwapinga, na afisa mazingira wilaya bi upendo wmesema kuwa miradi hiyo imekuwa chachu kubwa katika kukuza uchumi wa wanamakete, kutokana kuwepo kwa fursa mbalimbali za kilimo chenye tija, kama vile ufugaji samaki.

sauti ya afisa mifugo aldo mwapinga na afisa mazingira bi upendo

Naye mwenyekiti wa kikundi cha Tutunze Mazingira Ugabwa, Bi. Osilia Sanga, amesema kuwa, miradi ya ufugaji Samaki pamoja na Kilimo cha Ngano imekuwa na tija katika maisha yao, hivyo wameshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kuwakwamua kiuchumi.

sauti ya mwenyekiti wa kikundi tutunze mazingira bi osilia sanga

Nao baadhi ya wananchi kutoka kijiji cha ugabwa akiwemo onesmo mahenge pamoja na mtendaji wa kijiji cha ugabwa bi  Elimina chengula amewapongeza wanakikundi kwa ujumla kwa kuendelea kutunza mazingira na kuendeleza miradi katika maeneo hayo

sauti ya mwananchi na mtendaji wa kijiji ugabwa

Ikumbukwe kuwa, Mradi wa usimamizi endelevu wa matumizi ya ardhi ya Bonde la ziwa Nyasa umelenga Kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika bonde la Ziwa Nyasa ambao umetokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu, Shughuli hizo ni pamoja na; kulima kandokando ya kingo za mito na vyanzo vya maji, kulima katika miteremko ya milima, kujihusisha na Uvuvi haramu unaohusisha matumizi ya zana zisizoruhusiwa kisheria, kuchoma moto ovyo, kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa na kuni pamoja na kuchimba madini kwa njia isiyo endelevu.