Mwonekano wa moja ya Jengo la Chakula Mwakavuta Sekondari
Kitulo FM

RAS Njombe Aagiza Kukamilika Madarasa

August 15, 2023, 1:43 pm

Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kuhakikisha Ujenzi wa vyumba vya Madarasa, Bweni na Vyoo unakamilika kwa wakati kwa ajili ya mapokezi ya Wanafunzi Kidato cha Tano 2023.

Bi. Judica ametoa maagizo hayo akiwa Wilayani Makete tarehe 14 Agosti 2023 kwenye ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Madarasa, Bweni na vyoo ambavyo vinajengwa katika Shule ya Sekondari Matamba, Mwakavuta na shule ya wasichana Makete.

“Miundombinu hii ikamilike kwa muda uliopangwa na niwasihi kuwepo na mapokezi mazuri na yenye upendo kwa wanafunzi hawa ili waweze kufurahia Mazingira na wasome kwa Amani na kuyapenda mazingira ya upatikanaji wa Elimu”.

Hata hivyo, kufikia asubuhi ya leo Agosti 15, 2023 zaidi ya Wanafunzi 300 wameshaanza kuripoti, ambapo kati ya  wanafunzi 2,346, Wavulana ni 862 na Wasichana 1,485, ambao wanatakiwa kuanza Masomo yao katika shule mbalimbali Wilayani Makete.