Kitulo FM

makete yapiga hatua kila sesta miaka 61 ya uhuru 2022

December 9, 2022, 3:00 pm

makete ya piga hatua kila secta miaka 61 ya uhuru

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amesema maadhimisho  ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika ni msingi wa uhuru uliopatikana mara baada ya kutoka kwenye machungu makubwa ya utawala wa wakoloni ambao Taifa lilipitia.

Ameyasema hayo leo akiwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete wakati wa mdahalo ulioandaliwa na Halmashauri kwa lengo la kujadili maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 61 ya Uhuru

Mhe. Sweda amesema kama Taifa na jamii ya sasa ni vema kuendeleza tunu ya Amani, Upendo na mshikamano ambao Taifa limeachiwa na waasisi wa waliotanguli.

Mdahalo huo umehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa vyama vya Siasa, Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali, Viongozi wa Dini, Watendaji wa Kata, Wazee maarufu, walemavu, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa shule za Msingi na Walimu wakuu Sekondari, Wakuu wa Idara, Wenyeviti wa Vijiji na watendaji, wananchi pamoja na waandishi wa Habari

Awali akitoa salam za Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete William Makufwe amesema Makete inajivunia utekelezaji wa miradi mikubwa  inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania.

Pia ameongeza kuwa Wilaya inaendelea kuongeza fursa mbalimbali za Ajira kupitia sekta za uzalishaji ikiwemo Kilimo na kuhimiza wananchi kutumia Fursa zinazokuja ili kujiinua kiuchumi

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mdahalo huo wameipongeza Serikali kwa jitihada mbalimbali katika kusogeza huduma kwa wananchi ikiwemo Miundombinu ya Barabara, Maji, Elimu, Afya, Mawasiliano, Kilimo na Biashara

Kilele cha maadhimisho ya Uhuru imeenda sambamba na kauli mbiu “Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu”.