Dawa za P2 ni kwa ajili ya Dharura na si vinginevyo
Kitulo FM

Dawa za P2 si kila mtu anapaswa kuitumia

June 9, 2023, 7:51 am

Dawa aina ya P2 zimetengenezwa kwa ajili ya kumsaidia mama au binti kutopata ujauzito ambao hakutarajia na dawa hii ni aina  ya uzazi wa mpango inayotumika wakati wa dharura.

Dharura hizo kwa mwanamke kushiriki tendo la ndoa katika siku ambazo ni hatarishi kwakwe  kupata ujauzito kwa mfano kondom kupasuka, pindi mwanamke anapotumia njia ya kalenda na amekosea kuhesabu ama mwanamke  aliyebakwa.

Uwepo wa dawa hizi umekuwa na msaada kwa wanawake ama mabinti  ingawa kwa sasa umekuwa na madhara makubwa  kwa baadhi ya watumiaji kutokana na matumizi holela ya dawa hizi. Hapa mkaguzi wa dawa na vifaa tiba kutoka Mamlaka ya  Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA)  Jofrey Kikoti  anaeleza madhara hayo;

Bi. Krace Kapande ambaye ni mkaguzi wa dawa na vifaa tiba ameeleza hatua ambazo zinachukuliwa na TMDA baada ya tathmini ya madhara ya matumizi holela ya P2  ikiwemo kuishauri Wizara ya Afya kubadilisha sera ya dawa husika ndani ya nchi.

TMDA ni taasisi iliyo chini ya Wizra ya Afya inayosimamia udhibiti wa ubora , usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi nchini , mamlaka hii imeundwa chini ya sheria ya dawa na vifaa tiba sura ya 219.