Kitulo FM

GNM cargo yakabadhi madawati 40 kwa wanafunzi wa ilumaki sekondari

10 June 2026, 6:44 pm

baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa kwa wanafunzi wa sekondari ya ilumaki

ili kuendelea kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na kuweza kufikia ndoto zao, wazawa wa makete waishio nje ya makete wamekuwa wakihakikisha mazingira mazuri katika shule zote makete yanakuwa mazuri kwa kuendelea kutoa madawati kujenga mabweni ili wanafunzi wafurahie masomo yao kwa kusoma katika mazingira bora

na mwandishi wetu

Shule ya Sekondari Ilumaki iliyopo Kijiji cha Lupalilo Kata ya Lupalilo wilaya ya Makete Mkoani Njombe imepokea Jumla ya Madawati 40 kutoka kampuni ya Usafirishaji wa Mizigo GNM Cargo

Katika Makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya GNM Cargo Ndg Geofrey Nazareth Mbilinyi amesema wataendelea kutoa ushirikiano ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali katika Sekta ya Elimu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya GNM Cargo Ndg Geofrey Nazareth Mbilinyi akizungumza na wanafunzi wa ilumaki

Amewaasa walimu kutunza vyema madawati hayo kwani uhitaji wake ni mkubwa na pia wanafunzi kusoma kwa bidii na kutumia samani hizo vyema huku wakikumbuka malengo yaliyowapeleka shuleni huku akiwasisitiza wazawa wa makete waishio nje ya makete kurudi ili kuijenga makete iliyo bora.

sauti ya Mkurugenzi wa Kampuni ya GNM Cargo Ndg Geofrey Nazareth Mbilinyi

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Mhe. Rabson Mahenge amemshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya GNM kwa ushirikiano mkubwa ambao anatoa kwenye shughuli mbalimbali za Serikali sambamba na za Kijamii.

sauti ya mwenyekiti wa halmashauri mhe mahenge

wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na gnm cargo baada ya kupokea madawati hayo

Aidha Diwani wa Kata ya Lupalilo Ndug. Julton Sanga amesema Madawati hayo 40 yanaenda kutatua kero kubwa shuleni hapo kwani Wanafunzi watakuwa na Mazingira mazuri ya kusomea na kila mmoja akikaa kwenye Dawati lake.

diwani wa kata ya lupalilo jultoni

mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya makete mhe mahenge

Pia Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilumaki Mwl. Christoms Mturo kwa niaba ya Walimu amesema wataendelea kutimiza Wajibu wao kuhakikisha wanafundisha na kusimamia Nidhamu sambamba na Taaluma za Wanafunzi kwani ndio chachu ya Kujenga Taifa la kesho lililo imara.