Kitulo FM
Kitulo FM
22 June 2026, 9:57 am

dc kissa akizungumza mbele ya waumini katika Usharika wa Matamba uliopo Jimbo la Matamba
wito umeendea kutolewa kwa vijana na wananchi kwa ujumla kuendelea kuitunza amani na kudumisha upendo na mshikamano ili kuwa na taifa imara na lilobora
na mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Makete kissa gwakisa kasongwa jana Juni 21, 2026 ameshiriki Misa Takatifu katika Usharika wa Matamba uliopo Jimbo la Matamba, Dayosisi ya Kusini Magharibi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa akiwemo Askofu wa Dayosisi ya Kusini Magharibi, Stephen Edward Nguvila, Mkuu wa Wilaya ametoa mchango wa Shilingi Milioni Moja (1,000,000) kwa ajili ya kuunga mkono kazi na shughuli zinazoendelea katika Usharika wa Matamba.
Akizungumza na waumini wa kanisa hilo, Mkuu wa wilaya ya Makete amewataka washirika kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano katika jamii, akisisitiza kuwa usalama na utulivu ni msingi muhimu wa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
sauti ya mkuu wa wilaya makete kissa kasongwa
Askofu Stephen Edward Nguvila amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Makete kwa kushiriki ibada hiyo pamoja na mchango alioutoa kuunga mkono juhudi za ujenzi na maendeleo ya kanisa. Amesema ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na taasisi za dini una mchango mkubwa katika kuimarisha ustawi wa jamii.
Askofu Nguvila amewaasa Waumini wa Kanisa hilo kuepukana na Vikundi vyenye ushawishi na Dhamira ya kuvunja Amani kwenye Jamii, amesema Kanisa haliwezi fanya Ibada zake kama hali ya Usalama nchini haiko vizuri.

waumini wa Usharika wa Matamba wakiwa kwenye nyumba ya ibada
Mchungaji wa Usharika wa Matamba, Mchungaji Heri Nsemwa, amesema sadaka hiyo ni ishara ya moyo wa kujitolea na kuunga mkono maendeleo ya kanisa.
Ameongeza kuwa mchango huo uwe chanzo cha baraka katika uongozi wa Mhe. Kissa na chachu ya kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Makete.