Kitulo FM

DC Samweli Sweda aagiza Fundi kuongeza Kasi ujenzi wa Bwalo

October 7, 2023, 9:41 am

Dc Samweli Sweda akiwa eneo la ujenzi wa bweni picha na Furahisha Nundu

katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati mkuu wa wilaya ya Makete Mh:Samweli Sweda ametembelea miradi inayotekelezwa katika maeneo yote ya Wilaya ya makete Huku akitoa maagizo kwa watendaji na mafundi kukamilisha miradi hiyo kwa wakati

na Aldo Sanga

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amemuagiza fundi anayejenga Bwalo la Chakula Lupalilo Sekondari kukamilisha kwa wakati na kuongeza mafundi ili malengo ya Serikali yatimie kama yalivyopangwa

Maagizo hayo amaeyatoa leo Octoba 6, 2023 akiwa katika ukaguzi wa Jengo hilo sambamba na kiagiza Vifaa kununuliwa kwa wakati ili kitochelewesha ujenzi na kuacha visingizio

Serikali imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 198 kupitia Mpango wa Maendeleo TASAF ili kujenga Jengo la beni ambalo lilikwama kwa zaidi ya Miaka 10 tangu lianzishwe kwa nguvu za Wananchi wa Kata ya Tandala ambao walijenga Msingi na kushinda kuendelea

Jengo hilo kwa Sasa limefikia hatua ya kupandisha kuta na nguzo