Kitulo FM

Wananchi wahimizwa kufuata sheria pindi matukio ya uharifu yanapojitokeza

February 1, 2024, 6:31 pm

Imeelezwa kuwa elimu ni nguzo pekee ya wananchi kuweza kutambua sheria ili kufahamu haki na wajibu wao pindi ambapo wanapokuwa na changamoto mbali mbali pamoja na kutoa ushirikiano na vyombo husika katika kufanikisha haki inatendeka pindi ambapo uharifu unapojitokeza

Na Rose Njinile

Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Makete mkoani Njombe kuacha kujichukulia sheria mkononi pindi matukio ya kiuharifu yanapokuwa yamejitokeza katika jamii zao ili kuepuka uvunjaji wa sheria.

Hayo yamesemwa hii leo Februari Mosi 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo kiwilaya yamefanyika katika ukumbi wa Madiahan Villa Makete mjini.

Katibu Tarafa, Tarafa ya lupalilo ndg Agustino Ngailo akizungumza na wananchi kwenye wiki ya sheria

Katibu Tarafa, Tarafa ya lupalilo ndg Agustino Ngailo akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya makete mh Juma Sweda amesema kuwa kila mwananchi anawajibu wa  kutambua  namna bora ya kuweza kutambua sheria pindi matukio ya ukatili au uhalifu yanapotokea

Aidha ndg Ngailo amesema kuwa licha ya vitendo vya kikatili kuendelea kutokea katika jamii huku baadhi ya akina baba kufanyiwa vitendo hivyo vya kikatili wamesisitizwa kutonyamaza na badala yake watoe taarifa ili sheria ichukue mkondo wake

sauti ya katibu tarafa ndg ngailo

baadhi ya wanafunzi wa veta wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi

Hakimu mkazi mfawidhi mh Ivan Msack amewapongeza wadau Wa mahakama kwa kuendelea kushirikiana na mahakama katika utoaji haki huku maboresho yakiendelea kufanyika katika mahakama ili kuwa na miundombinu rahisi ya utoaji wa haki jinai na mwananchi aweze kupata huduma yake kwa haraka zaidi

sauti ya Hakimu mkazi mfawidhi mh Ivan Msack

Apolo laizer ni mwanansheria wa halmashauri ya wilaya makete kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ndg William Makufwe ameipongeza mahakama katika kuwahimiza wananchi kuendelea kuutumia muhimili wa mahakama  kutatua au kupata masaada wa migogoro mbali mbali inayojitokeza

sauti ya mwanansheria wa halmashauri laizer

Mwanasheri wa Halmashauri (w)Makete Apolo laizer akizungumza na wannachi kwenye wiki ya sheria

Rosemary Wambali akisoma Hotuba mbele ya mgeni rasmi kwaniaba ya wanachama wanasheria wa kujitegemea (TLS)amewaomba  wadau mbali mbali kuendelea kushirikiana na Tasisi zinazoshughulika  na haki  jinai ili kuweza kuhakikisha haki inapatikana kwa ustawi wa Taifa na wananchi kwa ujumla

sauti ya rosemary wambali wakili wakujitegemea

Kwa upande wa Mwendesha mashtaka wilaya ambaye pia ni inspekta wa jeshi la polisi Benstard Wwoshe akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi  amesema kuwa  utoaji na upatikanaji wa haki inawezekana ikiwa kutakuwa na  mfumo imara kama  vitendea kazi vya kisasa (TEHAMA),pamoja na uwepo wa miundombinu wezeshi baina ya taasisi za haki jinai

sauti ya mwendesha mashtaka wilaya benstard mwoshe

mwendesha mashtaka wilaya Benstard Mwoshe akitoa hotuba mbele ya mgeni rasmi na wananchi

Nao baadhi ya wadau mbali mbli wakiwemo Viongozi wadini, Shiriki la mapao, Takukuru, Veta, wamewasii wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye mahakama pamoja na vyombo vinavyohusika na uchunguzi ili haki iweze kupatikana huku wakiwasisitiza kuendelea kujitokeza katika sherehe hizo ili kupata elimu inayohusu sheria

Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo UMUHIMU WA DHANA YA HAKI KWA USTAWI WA TAIFA NAFASI YA MAHAKAMA NA WADAU KATIKA KUBORESHA MFUMO JUMUISHI WA HAKI JINAI