Viongozi wa Dini, Siasa na wazee maarufu wakiwa kwenye Kikao kuelekea uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kinyika
Kitulo FM

Viongozi vyama vya siasa, dini wafanya kikao kuelekea uchaguzi udiwani kata Kinyika

June 26, 2023, 7:20 am

Leo Juni 24, 2023 wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa ddiwani kata ya Kinyika wamekutana na kufanya kikao na viongozi wa vyama vya siasa wilaya ya Makete na kata ya Kinyika kwa lengo la kutoa elimu kuhusu uchaguzi kuanzia hatua za uchukuaji wa fomu, mchakato wa kuteua wagombea, upigaji kura na utangazaji wa matokeo.

Katika kikao hicho msimamizi wa uchaguzi jimbo la Makete ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe amewasisitiza viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi tangu kuanza kwa zoezi la uchukuaji wa fomu mpaka mshindi atakapopatikana baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 13 Julai 2023.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa (ACT-Wazalendo, CHADEMA na CCM), Viongozi wa dini na wazee maarufu kutoka vijiji vyote vya kata ya Kinyika.