Kitulo FM
Kitulo FM
8 June 2026, 8:00 pm

diwani wa kata ya iwawa mhe Rabson mahenge akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji
kutokana na baadhi ya watu kufanya shughuli za kilimo cha kutumia moto wakati wa kuandaa mashamba na hata kuvuna mbao kijiji cha ivalalila kimetunga sheria zitakazo saidia watu kuacha kuchoma moto misitu jambo ambalo limesababisha hasara ya fedha nyingi
na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Iwawa, Mfamasia Rabson Mahenge, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchoma moto ovyo katika maeneo yenye misitu na miti, akisisitiza kuwa miti ni rasilimali muhimu inayochangia maendeleo ya uchumi wa wananchi na wilaya ya Makete kwa Ujumla.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ivalalila kilichopo Kata ya Iwawa Mfamasia Mahenge amesema miti ina mchango mkubwa katika uchumi wa makete huku akisisitiza kuwa kwa Mwaka jana Makete imepata Hasara zaidi ya Bilioni 11 kwasababu ya uchomaji wa Misitu
diwani mahenge 01
Aidha diwani huyo wa kata ya iwawa amesisitiza kuwa yeyote atakaye choma moto misitu aweze kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria walizojiwekea huku akiwataka viongozi wa kijiji kuendelea kuyafanyia kazi yote waliyokubaliana kwenye mkutano huo ili wananchi waweze kuona hoja zao zinafanyiwa kazi
sauti ya diwani 02
Nae mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdg wa iwawa ndg Joseph Mbilinyi amesema kuwa kilimo cha misitu imekuwa ni tegemezi kwa wananchi wa makete na taifa kwa ujumla hivyo inapaswa kuendelea kuitunza na kuacha kuchoma moto
sauti ya joseph mbilinyi
Aidha Mwenyekiti wa Muungano Kijiji cha Ivalalila Ndg Razaro Chaula amesema wataendelea kuchukua Hatua za kisheria bila kusita dhidi ya wote wanaochoma Misitu ndani ya Kijiji hicho.
sauti ya mwenyekit kijiji chaula
Ikumbukwe ushirikiano wa jamii katika kulinda misitu ni muhimu kwa ustawi wa mazingira na maendeleo endelevu ya uchumi wa Wilaya ya Makete.