Kitulo FM

Serkali yatoa milioni 300 ujenzi madarasa, matundu ya vyoo Mount Chafukwe Makete

February 7, 2024, 5:36 pm

Ded William Makufwe (kushoto) akihojiana na mkuu wa shule ya Mount chafukwe picha na Lulu Mbwaga

Kiasi cha fedha milion miatatu (300,000,000) zitatumika kukamilisha ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa na matundu 20 ya vyoo ikiwa nikuendeleza juuhudi za wananchi katika kutika kuleta maendeleo kwa jamii hususani katika sekta ya elimu.

Na Lulu Mbwaga

Ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa na matundu 20 ya vyoo katika shule ya Sekondari ya Mount chafukwe iliyop kata ya mfumbi Halmashauri ya Wilaya ya Makete ikiwa gharama ya ujenzi wa vyumba hivo ni shilingi 36,000,000 na gharama za matundu ya vyoo ni shilingi 8,500,000

Mkuu wa shule hiyo akitoa taarifa ya mraji wa ujenzi wa madarasa na matundu ya vyooo

Baada ya mradi kukamilika wanatarajia ufaulu wa kidato cha kwanza mpaka cha nne kuongezeka zaidi kwani kidato cha Tano na sita wata wasaidia katika kujifunza kwa muda wa ziada na mradi utaongeza fursa za kiuchumi hususani ni usafirishaji wa wageni wanaokuja shule kutoka stendi ya kimani

Aidha shule hiyo imepokea kwa awamu nyingine shilingi Milioni 300,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo

Kamati ya fedha imeagiza ifikapo tarehe 20 mwezi 3 madarasa yawe yamekilika