Kitulo FM

PM Mwigulu amtaka mkandarasi barabara ya Makete-Mbeya kurejea kazini

16 November 2026, 10:48 am

Picha ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa barabara ya Makete -Mbeya ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na wakazi wa Makete, Waziri Mkuu ametoa majibu ya kwanini mradi umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu katika utekelzaji wake.

na mwandishi wetu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba,  leo Novemba 15,2026, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Makete – Mbeya kurejea kazini Ifikapo Novemba 19, 2026, kwakuwa Serikali ilishatimiza wajibu wake wa malipo ya ujenzi wa Miundombinu hiyo.

Mhe. Dkt. Nchemba,  amesema hayo kwenye  hafla ya Harambee ya Uchangiajia vifaa Tiba vya Hospitaliya KKKT – Bulongwa, ambayo imefanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo.

Aidha, katika hatua nyingine,  Waziri Mkuu Nchemba,  amesema kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa Fidia ambao umekuwa msaada mkubwa katika ulipaji wa madeni ya fidia, hivyo basi amewatoa hofu wakazi wa Bulongwa ambao wamefanyiwa Tathmini ya maeneo yao ili kupisha ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Lumakali. 

Sauti ya Waziri Mkuu

Mbunge wa jimbo la makete mhe Festo Sanga akizungumza mbele wa waziri mkuu na viongozi wengine kwenye harambee

Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga ametumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu kuharakisha ujenzi wa barabara ya Makete–Mbeya, akieleza kuwa hali ya barabara hiyo imekuwa ikiwasababishia wananchi kutumia hadi siku tatu wanaposafiri.

sauti ya mbunge Festo Sanga

Aidha,  Mbunge wa Jimbo la Makete,  Mhe. Festo Richard Sanga,  amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kufika Makete, hususan Kata ya Bulongwa ambayo imemkuza, na kuendesha harambee ya Upatikanaji wa Fedha ununuzi wa Vifaa Tiba, katika Hospitali ya KKKT – Bulongwa,  ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 1.07 zimepatikana.

Waziri mkuu akiwapungia mikono wananchi baada ya kuwasili kwenye viunga vya hospitali ya bulongwa

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki harambee hiyo, akiwemo Thobias Kyando amesema fedha zilizopatikana zitasaidia kununua vifaa tiba vya kisasa na hivyo kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu.