Kitulo FM
Kitulo FM
1 October 2026, 1:00 pm

Baadhi ya vijana ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10, wakiwa shambani, Picha na Benson Kyando
Kikundi cha Vijana cha Solidarity Forever cha Kata ya Mang’oto Kijiji cha Ilindiwe Wilayani Makete Mkoani Njombe, kimeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwawezesha mkopo wa asilimia kwa ajili ya kuwainua kiuchumi kipitia Kilimo.
Na. Rose Njinile
Kikundi cha Vijana cha Solidarity Forever kinachofanya shughuli zake za Kilimo katika Kata ya Mang’oto Kijiji cha Ilindiwe Wilayani Makete, Mkoani Njombe, kimeishukuru Serikali ya Jmahuri ya Muuungano wa Tanzania kwa kuwakopesha mkopo ya asilimia 10 ili uweze kuwainua kiuchumi kupitia kilimo cha viazi mviringo.
Kikundi hicho kimetoa shukrani hizo mara baada ya kutembelewa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bi Jackine Mroso, kwa lengo la kukagua Maendeleo ya kikundi hicho kupitia kilimo cha viazi mviringo katika kijiji cha Ilindiwe, kilichopo Kata ya Mang’oto.

Mwonekano wa Shamba la wanufaika kwa mkopo wa Asilimia 10, lililopo katika Kijiji cha Ilindiwe.
Akizungumza Shambani hapo, Bw. Antony Cleva ambae ni mjumbe wa kikundi hicho cha Solidarity Forever amesema kuwa mkopo huo umeedna kuwainua kichumi kwasabau wameupata wakati sahihi kulingana na Hali ya Hewa ya eneo hilo ambayo inaruhusu kufanya kilimo kwa sasa.
Sauti ya Mnufaika na mkopo waasilimia 10, Bw. Antony Cleva
Aidha, Bw. Cleva, ameisihi Serikali kuendelea kutoa mikopo hiyo kwasababu imekuwa na tija kwa wananchi wa kawaidia ambao hawawezi kupata mikopo hiyo kupitia taasisi za kifedha, kwakuwa zimekuwa zikihitaji dhamana kubwa ambayo mananchi wa kawaida hawezi kuimudu.

Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi.Jackline Mroso amewataka wanakikundi hao kuendelea kushirikiana vizuri ili waweze kutimiza malengo yao kwa wakati, huku akiwataka kuzitumia vizuri fedha hizo wanazozipata ikiwa ni pamoja na kuzirudhisha kwa wakati.
Ikunbukwe kuwa, Kikundi cha Vijana cha Solidarity Forever kilichopo katika Kijiji cha Ilindiwe, Kata aya Mang’oto kimekopeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Makete kiasi cha shilingi milioni 40, kupitia makusanyo ya mapato ya ndani.