Kitulo FM

Wajawazito Makete watakiwa kutumia Vidonge vyenye Virutubishi

2 October 2026, 4:07 pm

Pichani ni Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi. Jackline Nanauka, akitoa mafunzo kwa wakazi wa kijiji cha Malembuli (Hawapo Pichani), Kata ya Mang’oto juu ya umuhimu wa Lishe Bora kwa watoto na Mama Mjamzito.

Halmashauri ya Wilaya ya Makete, kupitia Idara ya Aya, (Kitengo Lishe), Oktoba 1,2026, imetoa elimu ya umuhimu wa kutumia Vyakula vilivyoongezwa Virutubishi vya Madini na Vitamini kwa wananchi wa Kijiji cha Malembuli, Ilindiwe na Shule ya Msingi Malembuli.

Na. Ombeni Mgongolwa

Halmashauri ya Wilaya ya Makete, kupitia Idara ya Aya, (Kitengo Lishe), Oktoba 1,2026, imetoa elimu ya umuhimu wa kutumia Vyakula Vilivyoongezwa Virutubishi vya Madini na Vitamini kwa wananchi wa Kijiji cha Malembuli, Ilindiwe na Shule ya Msingi Malembuli ili kuhakikisha kuwa wananchi wakuwa na uelewa mzuri wa umuhimu wa Lishe Bora.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete , Bi. Jackline Nannauka, amesema kuwa, mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa pamoja na mapambano dhidi ya Udumavu Wilayani humo.

Pichani ni Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, wakatia akitoa Elimu ya madhara ya kutotumika vidonge vya virutubishi kwa wakazi wa Kijiji cha Malembuli.

Sambamana na mafunzo hayo, Bi. Jackline amesema kuwa, elimu hiyo pia imelenga uhamasishaji wa Matumizi ya Virutubishi Mchanganyiko kwa Wajawazito, pamoja na madhara endapo watashindwa kutumia Virutubishi hiyo pamoja na elimu ya Usafi wa Mazingira.