Kitulo FM
Kitulo FM
5 November 2026, 10:05 am

mwenyekiti wa Redcross Mkoa wa Njombe Edgar Bosco Mtitu akizungumza na wanachama wa red cross makete
kutokana na tahadhari inayotolewa kuhusu mvua za el nino pamoja na majanga mengine shirika la msalaba mwekundu makete wamesisitizwa kuendela kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujinga na majanga hayo
na Rose Njinile.
Mkuu wa wilaya ya makete mhe Kissa Gakwisa Kasongwa amewataka wanachama wa Red cross wilaya ya makete kuendelea kuwahudumia jamii kwa utu na kwa kujitoa huku akiwasisitiza kujitokeza kwenye fursa mbali mbali zinazojitokeza kwenye maeneo yao
Mhe Kissa Kasongwa ameyasema hayo kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa uliokuwa na lengo la kutambulisha uongozi mpya wa red cross mkoa wa Njombe pamoja na kumchagua mratibu wa red cross wilaya ya makete
sauti ya dc kissa Kasongwa 01
Mwenyekiti wa Redcross Mkoa wa Njombe Edgar Bosco Mtitu amewahimiza wanachama hao kuendelea kufuata misingi ya red cross katika kuhakikisha wanahamasisha jamii kuchangia damu, kupinga ukatili wa kijinsia kuwa waadilifu,kujitolea pamoja na kuwa na umoja na hata kufanya matendo ya huruma kwenye jamii
sauti ya Mwenyekiti wa Redcross Mkoa wa Njombe Edgar Bosco Mtitu 02

baadhi ya wananchama wa msalaba mwekundu wilaya ya makete
Aidha Ndg Edgar amewasisitiza kuwa na mipaka ya sare za red cross na kuepuka kuvunja miiko ya taasisi hiyo kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume kwa kutokujihusisha kwenye matukio mabaya kama ugomvi kambi za starehe huku ukiwa umevalia sare yenye nembo ya red cross kwakuwa kosa hilo adhabu yake ni kifungo
sauti ya wenyekiti wa red cross Edgar 03
Nae Diwani wa kata ya iwawa Mhe Rabson Antony Mahenge amewasisitiza wanachama hao wa red cross wilaya ya makete kujitoa na kuonekana kwa jamii ili uongozi uweze kuwatumia katika shughuli mbali mbali ambazo zinaweza kujitokeza katika halmashauri ya wilaya ya makete
sauti ya diwani kata ya iwawa mhe Rabson 04

Mwenyekiti wa Redcross Mkoa wa Njombe Edgar Bosco Mtitu akiendelea kuzungumza na wanachama wa red cross
Mratibu wa Red Cross Mkoa wa Njombe ndg Cyprian Madege amesema kuwa lengo pia lakufika makete ni kuendela kutoa tahadhari kwa wananchama wa red cross kuhusu mvua za El Nino ili waweze kwenda kwa jamii kutoa elimu namna ya kujiandaa na kujikinga dhidi ya mvua hizo zinazotarajiwa kuanza mwezi oktoba mwaka huu
sauti ya mratibu wa red cross mkoa Madege 05
Hata hivyo mratibu huyo amebainisha majukumu makubwa ya red cross katika jamii kuwa ni pamoja na kutoa huduma ya kwanza kwa jamii hasa kwenye mikusanyiko ya watu wengi kama mikutano, kutoa elimu mbali mbali ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko,kutoa elimu ya kujikinga na maafa pamoja na kuhamasisha jamii kujitolea kutoa damu salama
Nao baadhi ya wanachama wa red cross akiwemo bi fungo wameshukuru kwa uongozi huo mpya wa mkoa wa njombe kufika katika halmashauri ya makete huku wakisema kuwa ujio wao utaongeza chachu kwao katika kuendesha gurudumu la kusaidia shughuli mbali mbali
sauti za wanachama 06
Uongozi wa red cross mkoa wa njombe umesema umelichukua jina lililopendekezwa na wanachama hao la chriss Patrick sanga kuwa mratibu wa red cross makete ili taratibu zingine zifanyike na kuweza kuanza kutekeleza majukumu yake