Kitulo FM
Kitulo FM
7 October 2026, 8:00 pm

mbunge wa jimbo la makete Mhe Festo Sanga akiwa na baadhi ya viongozi wa kata ya Tandala kwenye mkutano wa hadhara
Kwa mujibu wa sensa 2022 makete wapo watu 109,000 idadi ambayo iko chini huku baadhi ya shule za msingi zikiwa na wanafunzi wachache licha yaserikali kuboresha miundombinu ya shule
na Edwin Moshi
Wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitafakari kutokana na kuendelea kupungua kasi ya wao kuzaliana kwa kuwa suala hilo lina athari kwenye Maendeleo
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga akiwa kwenye kijiji cha Usagatikwa kata ya Tandala ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kijiji kwa kijiji

baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la makete
Mbunge Sanga amesema wananchi wengi wa Makete wanatakiwa kuachana na uzazi wa mpango na badala yake wazaliane kwa wingi kwani linapokuja suala la maendeleo, kigezo cha idadi ya watu nacho kinaangaliwa hivyo kama mpo watu wachache maendeleo yatachelewa kufika
Katika hatua nyingine wananchi hao wamekubaliana na mbunge kuwa matumizi ya uzazi wa mpango, ugumu wa maisha, wanaume kutelekeza wake zao na kujiweka kando kwenye suala la malezi ni miongoni mwa sababu zinazopelekea wananchi wa Makete kupunguza kasi ya kuzaliana
Amesema pamoja na hayo kama wananchi wanataka maendeleo makubwa wanapaswa kuzaliana kwa wingi kwa kuwa changamoto zozote zinazojitokeza wanatakiwa kuzitatua na si kukwepa kuzaliana.
sauti ya mbunge Festo Sanga 01
Hata hivyo mbunge huyo amesema kuwa wapo baadhi ya wanawake wanatumia uzazi wa mpango bila kuwashirikisha wenza wao jambo ambalo limekuwa likisababisha kutokuelewa na wenza wao huku akiwasisitiza vijana pia kuacha kutumia pombe kupita kiasi kwa kuwa ni hatari kwa afya zao
sauti ya mbunge Sanga 02
Mhe sanga anaendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi