Kitulo FM

Makete : Watupa taka hovyo kupewa adhabu kali

1 October 2026, 3:51 pm

Pichani ni mmoja wa wananchi waliojitokeza katika siku ya ufanyaji Usafi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Picha na Edwin Moshi.

Wananchi wa Vijiji cha Ikonda na Tandala vilivyopo Wilayani Makete mkoani Njombe, wametakiwa kutoa taarifa za uchafuzi wa mazingiria ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwa ni mwendelezo wa kuweka mazingira safi.

Na. Rose Njinile

Wananchi wa Kijiji cha Ikonda na Tandala Wilayani Makete mkoani Njombe, wametakiwa kutoa taarifa za uchafuzi wa mazingiria ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwa ni mwendelezo wa kuweka mazingira safi.

Hayo yamebainishwa Diwani wa Kata ya Tandala, Mhe. Ignatio Mtawa, wakati akizungumza na wanachi hao wakati wamejitokeza katika kufanya usafi wa kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi, ambapo kiwilaya yalifanyika katika Kijiji cha Ikonda, kilichopo Kata ya Tandala.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Tandala, akizungumza umuhimu wa ufanyaji usafi katika mkutano na wananchi

Aidha, Mhe. Mtawa, amewataka wananchi kukemea tabia ya wizi ambayo imeonekana kuibuka katika siku za karibuni kwenye vijiji vya Ikonda na Tandala, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo husika ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kulinagana na makossa yao.

Sauti ya Diwai wa Kata Mhe. Ignatio Mtawa, akizungumza na wananchi kuhusu wizi uliokithiri

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara Soko la Kijiji cha Tandala Bw. Enord Betweli amesema wataendelea kuzingatia suala la usafi katika maeneo mbalimbali ya mji huo, na kuomba serikali kuendelea kuboresha mazingira yatakayorahisisha zoezi hilo ikiwemo uwepo wa vifaa vya kutupia taka.

Diwani wa Kata ya Tandala akizungumza na wananchi mara baada ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Kijiji cha Tandala.

Sambamba na hayo, wananchi wa Kata hiyo ya Tandala, wamekumbushwa kuchukua tahadhari ya mvua za El Nino ikiwemo kufungua mifereji ya maji pamoja na kuacha kutupa takataka kwenye maeneo yasiyoruhusiwa hasa kwenye miti.