Kahama FM

Wafanyabiashara Kahama, wasisitizwa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozizalisha

18 November 2026, 11:01 am

Katibu Tawala Wilaya ya Kahama Glory Absalum, akizungumza katika Hafla ya Ufunguzi wa Viwango Clinic inayoendeshwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wilaya ya Kahama (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘TBS yafungua viwango clinic kahama na kutoa elimu ya ubora ya bidhaa’’

Wafanyabiashara wa Chakula na Vipodozi katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya biashara kwa kiwango kinachokidhi Miongozo ya kisheria ili kulinda Afya ya Mtumiaji.

Rai hiyo imetolewa Leo na Katibu Tawala Wilaya ya Kahama Glory Absalum, wakati akizungumza katika Hafla ya Ufunguzi wa Viwango Clinic inayoendeshwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa Wilaya ya Kahama akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt Francis Daud.

Glory amewasisitiza Wafanyabiashara kuhakikisha Wanasajili Maduka yao au Biashara zao kwa mujibu wa Sheria, lakini pia kutambua bidhaa zinakozalishwa ili zisilete athari kwa Watumiaji wakati Serikali ikisimamia Sheria ya ubora.

Sauti ya Katibu Tawala Wilaya ya Kahama Glory Absalum

Kwa upande wake Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi Joseph Makene, amesema Clinic hiyo ni fursa kwa Wananchi kukutana na Wataalam wa TBS kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na Shirika hilo.

Sauti ya Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi Joseph Makene

Baadhi ya Wafanyabiashara wakizungumza wamesema ni muhimu biashara zikafanyika kwa kuzingatia Mwongozo unaosimamia Viwango vya ubora wa bidhaa, ili kuepuka athari kwa mlaji na Mtumiaji.

Sauti mbalimbali za wafanyabiashara wa wilaya ya Kahama

Viwango Clinic imeanza tarehe 16 hadi 20 Novemba 2026, ambapo Wafanyabiashara na Wananchi Wilayani Kahama wanapata huduma mbalimbali ikiwemo Ushauri kuhusu Viwango na ubora, Elimu ya bidhaa salama na ubora, Taarifa za huduma nyingine za TBS, Mwongozo na uidhinishaji alama ya Viwango pamoja na usajili wa bidhaa na Majengo ya Chakula na Vipodozi.