Kahama FM

Kahama kuwa mji wa kisasa, mpango wa kidigitali kutumika

3 June 2026, 5:20 pm

Afisa mipango miji kutoka kampuni ya Urban Solution Elias Nyabusani akizungumza na wananchi wa kata ya Zongomera (Pichs nsSebastian Mnakaya)

”Wananchi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wako tayari kwa mabadiliko ya mji wa Kahama kuwa wa kisasa ifikapo 2050”

Wananchi wa kata Zongomera, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi wa mpango kabambe wa kidigitali, utakaokwenda kuboresha maeneo yao ya makazi kwa kupangwa katika mpangilio mzuri na wakisasa.

Wakizungumza leo viongozi mbalimbali wa kata hiyo kwenye mafunzo ya siku moja ya namna ya mradi huo wa Mpango Kabambe wa kidigitali utakavyotekelezwa katika Manispaa ya Kahama chini ya mradi wa uboreshaji wa miji nchini (TACTIC).

Baadhi ya wananchi wa kata ya Zongomera, akiwemo Marietha Richard na Daud Sasa, wamesema kuwa kuwepo kwa mradi huo utasaidia makazi yao kuwa bora na yenye thamani baada ya kutengenezwa kwa miundombinu mbalimbali kupita mradi huo.

Aidha, wananchi hao wameiomba serikali kupitia mradi huo, kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara kwa kujenga mitaro na barabara kuweza kupitika, huku wakiwaomba wananchi kutoa ushirikiano pale ambapo patahitajika wananchi kupisha ardhi kwa ajili ya shughuli za kijamii.

Sauti za wananchi wa kata ya Zongomera Marietha Richard na Daud Sasa

Kwa upande wake, afisa mipango miji kutoka kampuni ya Urban Solution Elias Nyabusani amesema mradi huo unawashirikisha wananchi moja kwa moja kwa kutoa maoni yao ili yaingizwe kwenye mpango na kuanza kutekelezwa kwake.

Sauti ya afisa mipango miji kutoka kampuni ya Urban Solution Elias Nyabusani

Hata hivyo, baada ya miaka 25 ijayo Kahama itakuwa ni mjini wa kisasa na wa mfano katika manispaa nyingine zote chini, huku mradi huo ukitekelezwa kwenye kata zote 20 katika manispaa hiyo.