Kahama FM
Kahama FM
6 June 2026, 1:32 pm

‘‘Lipeni wakulima katika mfumo wa njia ya simu ama benki na si kwa njia ya mkononi kama ilivyo sasa’’
Wakulima wa zao la Pamba mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya malipo yao wa kutumia mfumo wa kidigiti ili kuondokana na upotevu fedha unajitokeza kila msimu wa kilimo, kutokana na kutumia mfumo wa kulipa fedha mkononi (Cach).
Agizo hilo limetolewa leo Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julias Mtatiro akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, wakati wa mkutano wa Jukwaa la Maendeleo la Ushirikia mkoani humo.
Aidha, Mtatiro amewataka wakulima pamoja na viongozi wa vyama vya msingi vya zao la Pamba kubadilika na kutumia mfumo mpya wa malipo kwa kutumia benki na simu katika kufanya malipo ili kuondokana upotevu wa fedha hizo.

Kwa upande wake Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga,Kakozi Ibrahim, akiwasilisha taarifa ya hali ya ushirika mkoani Shinyanga amesema kuwa kuuza pamba kupita mfumo wa fedha tasilimu, umekuwa ukipoteza fedha nyingi na kutawataka kutumia mifumo ambao utaondoa changamo hiyo.

Awali, Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa ShinyangaEmanuel Nyambi, amesema kila mwaka wamekuwa wakipata hasara kutokana na vyama vya msingi kutumia mifumo wa kulipa wakulima kwa fedha tasilimu, na kuwaomba katika msimu wa kilimo watumie kwa njia ya simu ama benki.

Naye, mkaguzi wa zao Pamba wilaya ya Kahama Emmanuel Kileo amesema kuwa bodi ya pamba imetoa muongozo mpya ambao, kila chama cha msingi cha wakulima wa zao hilo, wanapswa kulipwa fedha zao kwenye mfumo wa simu na benki.
Hata hivyo, Jukwaa la Maendeleo la Ushirika mkoa wa Shinyanga tangu kuanzishwa kwake leo wamefanya mkutano wa 4 kwa kauli mbiu ‘‘Linda Ushirika, Chagua Uadilifu’’