Kahama FM

Zaidi ya wakulima 1,092 wadai ruzuku ya mbolea Ushetu

11 May 2026, 3:17 pm

Diwani wa kata ya Bukomela Kulwa Shoto (Picha na Sebastian Mnakaya)

Zaidi ya wakulima 1,092 katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wanadai ruzuku ya mfuko wa pembejeo aina ya NPK kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 125.

Madai hayo yametolewa na Diwani wa kata ya Bukomela Kulwa Shoto katika kikao cha baraza madiwani katika hali mashauri hiyo, ambapo amesema kuwa mpaka sasa wakulima hao wajalipwa fedha hizo na kuomba mamlaka husika kulipa fedha hizo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bukomela Kulwa Shoto
meneja shughuli kutoka chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Amri mwinyi mkuu

Akitoa ufafanuzi juu ya madai hayo, meneja shughuli kutoka chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Amri mwinyi mkuu, amesema mpaka sasa wakulima 2,809 hawajalipwa fedha hizo za ruzuku, huku wakipokea taarifa hiyo na kuifanyia kazi ili waweze kulipwa.

Sauti ya meneja shughuli kutoka chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Amri mwinyi mkuu
mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gigi Lala

Kwa upande wake, mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gigi Lala amekitaka chama ushirika KACU kushugulika jambo hilo kwa haraka ili wakulima walipe fedha hizo.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gigi Lala